Dk Mpango: Vijana msitoe figo

 

VIJANA wametakiwa kuacha tabia ya kuuza viungo vyao vya mwili ikiwemo figo ili kuepukana na madhara ya kiafya.

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ametoa wito huo akiwa ziarani mkoani Ruvuma mara baada ya kuzindua jengo la kutolea huduma ya usafishaji figo lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph–Peramiho.

Dk Mpango amesema utoaji wa figo unaweza kuhatarisha maisha hususani figo iliyobaki inaposhindwa kufanya kazi kwa ufanisi.

Aidha, amewataka watanzania kuwa na utaratibu wa kupima afya ili kuepukana na hatari za maradhi mbalimbali na kufikia hatua mbaya zaidi.

Dk Mpango ameshauri kuachana na ulaji usiofaa, unywaji wa pombe kupitiliza pamoja na kuhimiza kufanya mazoezi kuepukana na hali hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments