Mbunge Kishoa apanda jukwaa la CCM akimfagilia Rais Samia

Mbunge wa Viti Maalum Jesca Kishoa amesema Tanzania imejaliwa kuwa na Rais mvumilivu asiye na mfano.

Kishoa ambaye ni mbunge kutoka kundi la wabunge 19 wa chadema ametoa kauli hiyo Jana Jumapili Julai 23, 2023 kwenye mkutano wa kanda wa CCM unaofanyika uwanja wa bombadia mjini Singida.

Mkutano huo uliongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ukibeba kauli mbiu ya ‘Uwekezaji kwenye bandari ni ufunguo muhimu Kwa uchumi na Maendeleo yetu’ ulihudhuriwa na wana CCM wa Mikoa ya Dodoma, Tabora na Wenyeji Singida.


"Mungu ametupendelea kutupa Rais mvumilivu sana, mama huyu ametupa heshima kubwa sisi wanawake na ninaomba kila mahali mama huyu tumuombee," amesema Kishoa.

Ametaja baadhi ya mambo ambayo amedai Rais Samia ameiheshimisha nchi ni sekta za madini na utalii kwamba zimekuwa zikifanya kazi.

Mbunge huyo amepandaa jukwaani akikaribishwa na Mbunge wa Ukonga, Jelly Silaa na alipopanda jukwaa aliwasalimu washiriki wa mkutano kwa salamu ya kidumu Chama Cha Mapinduzi ambayo ndiyo salamu za chama hicho.

Hata hivyo siyo mara ya kwanza Kishoa kumsifia Rais Samia Suluhu Hassan kwani katika mkutano wa bunge uliokwisha alipeleka bungeni wageni mara mbili ambao walitambulishwa kama ‘chawa wa mama’.

                  


                     

                     

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments