KLABU ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Luis Jose Miquissone kwa mkataba wa miaka mitatu.
Winga huyo raia wa Msumbiji, aliwahi kuitumikia Simba kabla ya kuuzwa Al Ahly ambayo nayo ilimtoa kwa mkopo kabla ya kutangazwa tena kurejea Simba.
Simba sasa imekamlisha usajili wa wachezaji, Che Malone, Shabani Iddi, Fabrice Ngoma, Abdallah Hamis, David Kameta, Essomba Onana na Aubin Kramo.
0 Comments