MNEC Mkoa wa Singida Bw.Yohana Msita na Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida Leo Tar. 26.07.2023 ikiwa ni siku ya pili ya ukaguzi wa Miradi katika Utekelezaji wa ILANI ya Chama cha Mapinduzi - CCM, Wilaya ya Mkalama, Kamati hiyo imeagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya Wanawake na Wanaume katika hospitali ya wilaya ya Mkalama, baada ya wodi hizo kufikisha miaka mitatu bila kukamilika.
Kamati hiyo ya siasa mkoa wa Singida inafanya ziara hiyo kwa lengo la kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita ili kubaini hatua za miradi hiyo ilipofikia na changamoto zinazoikabili ili kutoa ushauri na maagizo ya kuhakikisha miradi hiyo inatoa huduma kwa wananchi.
Kamati hiyo pia imetembelea Kikundi cha wanawake Songambele, Shule Mpya ya Nkindoko na Kukagua ujenzi wa Barabara ya Ulemo Gumanga.
Aidha Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida imewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mkalama kuhakikisha wanatembelea na kutoa Elimu kwa Vikundi vinavyojishughulisha na uzalishaji ili viendelee kuwa hai na vyenye tija kwa wahusika wa vikundi na jamii kwa ujumla.
Hata hivyo Wananchi wa Wilaya ya Mkalama wametakiwa kuchangamkia fursa ya upatikanaji wa umeme katika maeneo yao kwa kufanya shughuli za maendeleo.
Rai hiyo imetolewa mara baada ya kamati hiyo kukagua Mradi wa REA katika kitongoji cha Sokoni kilichopo kijiji cha Mwando.
MNEC amempongeza Rais Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi katika Miradi ya wananchi.
Na Abdul Bandola
0 Comments