Mwenyekiti CCM Mkoa Wa Singida Kuwasha Moto Katika Ziara Yake Ya Kikazi Kesho Wilaya Ya Singida Mjini

                

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Singida,  Bi.Martha Mlata (pichani) kesho Julai 3, 2023, anatarajia kuwasha moto wakati atakapo kuwa katika ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Singida ya kukagua miradi ya maendeleo na  kuzungumza na wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Shabani Hamisi alisema ziara hiyo katika wilaya hiyo ni ya muhimu sana kwao.

"Ziara hii aatakayoianza tarehe 03 Julai 2023 mwenyekiti wetu wa chama mkoani hapa ni ya muhimu sana kwa ajili ya kukiimarisha chama," alisema Hamisi.

Akizungumzia mambo atakayoyafanya wakati wa ziara hiyo alisema atatembelea Balozi Shina namba tisa lililopo Kitongoji cha Mnung'una ambapo pia atapata nafasi  ya kuzungumza na wananchi wakiwemo Wana CCM na kupata taarifa ya chama.

Alisema kazi nyingine ambayo ataifanya ni kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo na moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa shule za Boost uliopo  Kata ya Minga na ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata hiyo.

Hamisi alisema katika ziara hiyo Mlata ataongozwa na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya hiyo chini ya Mwenyekiti Lusia Mwiru.

Mwenyekiti  wa chama mkoani singida Bi.  Martha Mlata ataendelea na ziara hiyo katika wilaya ya Mkalama atakayoifanya Julai 4, 2023, Iramba, Julai 5, Ikungi Julai, 6, Singida Vijijini, Julai 7 na kumalizia katika Wilaya ya  Manyoni Julia 8 na 9.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments