Rice kutangazwa Arsenal leo

Klabu ya West Ham United imesaini karatasi za mauzo ya £105m kwa Declan Rice kwenda Arsenal.

Mtandao wa Sky Sports umeeleza kuwa baada ya kitendo hiko ‘The Gunners’ wanatarajia kutangaza makubaliano kabla ya ziara ya Marekani Jumapili.

West ham ‘The Hammers’ walikubali uhamisho huo siku nane zilizopita ila walikuwa hawaelewi kinachochelewesha kukamilisha dili hilo.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, timu hizo mbili zitatangaza kuuziana mchezaji huyo leo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments