TMA yatahadharisha uwepo wa El Nino Oktoba

Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania (TMA) imesema El Nino inatarajiwa kuwepo katika kipindi cha mvua za msimu wa vuli zitakazoanza kunyesha Oktoba hadi Desemba mwaka huu ambazo zitasababisha athari katika maeneo mbalimbali nchini.

Akitoa taarifa hiyo leo Jumatano Julai 19, 2023 Meneja wa Utabiri wa TMA, Dk Mafuru Kantamla amesema hadi kufikia sasa inaonyesha imefikia asilimia 90 ya kuwepo kwa El Nino hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Dk Kantamla aliyataja maeneo ambayo yataathirika na mvua za El nino ni mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.

"Ongezeko la mvua linasababisha kutabiri uwepo wa El Nino, mfano kipindi cha kipupwe tumeona imeanza kujitengeneza athari zake hatutegemei kipindi hiki ongezeko la mvua kubwa,"amesema Dk Kantamla.

Pia, Dk Kantamla amesema El Nino haitaathiri wakazi bahari ya hindi pekee itasambaa hadi maeneo ya nyanda za juu Kaskazini na ukanda wa Pwani.

“Katika kipindi hiki cha kipupwe TMA inaendelea kufuatilia kwenye mchakato wa kuelekea msimu wa mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza Oktoba hadi Desemba mwaka huu na kuangaliwa athari za El Nino kwa ufasaha Ili kuifahamisha jamii kwa ujumla,”amesema.


Nini maana ya El Nino

Ni hali ya uwepo wa ongezeko la joto la bahari ya katika eneo la kati ya kitropiki la bahari ya Pasifiki, hali hii inapokuwepo kunakuwa na madhara mbalimbali katika maeneo tofauti ya duniani.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments