Recent-Post

VIJANA CHANGAMKIENI FULSA ASEMA YOHANA MSITA MNEC MKOA WA SINGIDA

               

 Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Singida imeridhishwa na Utekelezwaji wa Miradi mbalimbali katika wilaya ya Ikungi kupitia ILANI ya Chama cha Mapinduzi - CCM.


Kamati hiyo imeridhishwa baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi hiyo wilayani Ikungi, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara hiyo baada ya kukagua miradi katika wilaya ya Manyoni na Mkalama.

Ikiwa katika kikundi cha vijana cha kilimo cha umwagiliaji, YOHANA MSITA ambaye ni MNEC wa mkoa wa Singida amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali za kuwezesha vikundi vya Ujasiriamali.

MSITA aliwataka vijana ambao wana vikundi vya uzalishaji mali kutumia fedha wanazozipata kwa matumizi sahihi,Na kamati ya siasa imepongeza TANESCO kwa kutekeleza maigizo ya chama na serikali kwa kufikisha umeme kwenye mradi wa kilimo Cha umwagiliaji choda

Aidha kamati hiyo ya Siasa Mkoa wa Singida imetembelea Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Sekondari Ikungi na Shule ya Msingi Matare na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Madarasa katika Shule hizo.

Hata hivyo kamati hiyo ya siasa mkoa wa Singida imekagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Samaka, ambapo hapo kamati ilitoa wito wa kumalizia ujenzi wa Zahanati hiyo ili wananchi waanze kupata huduma za afya karibu na maeneo yao.

Kwa upande wao wananchi wa Kijiji cha Samaka wameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kujenga Zahanati hiyo itakayowasaidia kupunguza changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya, hali ambayo ni hatari kwa akina Mama wajawazito na Watoto.

Matukio Mbali mbali ya Picha katika ziara ya kamati ya siasa mkoa wa singida Iliyokuwa ikiongzwa na Mnec wa mkoa Wa Singida Bw. Yohana Msita 
Na Abdul Bandola Singida

Post a Comment

0 Comments