Recent-Post

Aliyeshiriki kuchanganya udongo wa Tanganyika, Zanzibar afariki


 Khadija Abbas Rashid (74) miongoni mwa walioshiriki kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar amefariki dunia jana Jumanne Agosti 23, 2023 nyumbani kwake Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano ambapo wametoa taarifa hiyo katika mitandao yao mbalimbali ya kijamii.

Marehemu alihusika katika tukio hilo la mfano la kuchanganya mchanga Aprili 26, 1964.

Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Julius Nyerere na Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na Abeid Karume ziliungana na kuunda Tanzania.

Post a Comment

0 Comments