Benki Ya NBC Yakabidhi Basi Jipya Lenye Thamani Ya Sh Ya Mil 470 Kwa Klabu Ya Singida Fountain Gate FC.

 Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League imekabidhi basi jipya kwa timu ya Singida Fountain Gate FC ya mkoani Singida inayoshiriki ligi hiyo ikiwa ni mwendelezo wa dhamira ya dhati ya benki hiyo katika kuboresha ligi hiyo.


Singida Fountain Gate FC inakuwa klabu ya pili inayoshiriki ligi hiyo kunufaika na mpango huo unaohusisha mkopo nafuu kutoka benki hiyo baada ya klabu ya KMC ya kinondoni kunufaika na mpango kama huu mwezi Februari mwaka huu.

Hafla ya makabidhiano ya basi hilo lenye thamani ya sh ya milioni 470 imefanyika jana kwenye Uwanja wa CCM Liti, Mkoani Singida ikihisisha viongozi waaandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru sambamba na Rais wa Klabu hiyo Bw Japhet Makau, ikienda sambamba na shamramshara za maadhimisho ya siku ya Singida Big Day zilizofanyika viwanjani hapo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Ndunguru alisema basi hilo ni sehemu ya mpango wa utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo ambapo klabu ya Singida Fountain Gate FC inatakiwa kurejesha mkopo huo ndani ya miaka miwili ukiwa na riba shindani katika soko.

‘’Basi hili ni ‘brand new’ la mwaka 2023, na limekatiwa bima na Benki ya NBC ambayo ina cover usalama wa abiria wote ndani ya gari na bima inatumika kwa nchi za Africa Mashariki na kati (Comesa). Gari limenunuliwa toka kampuni ya Africarriers Co. Ltd ya jijini Dar likiwa na uwezo wa kubeba abiria 58,’’ alifafanua Ndunguru.

Kwa mujibu wa Bw Ndunguru ukosefu wa vyombo vya usafiri maalum kwa ajili ya timu zinazoshiriki ligi hiyo imekua ni moja ya chanzo cha vikwazo vingi katika gharama za uendeshaji na utendaji wa timu husika.

“Zaidi pia NBC tunaendelea kushirikiana kampuni washirika wa huduma za Bima wa Sanlam na Britam inatoa huduma za bima za afya na maisha kwa wachezaji wote wa timu zinashiriki ligi kuu ya NBC , mabenchi ya ufundi pamoja na familia zao.’’ Aliongeza.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Rais wa Klabu hiyo Bw Japhet Makau pamoja kuishukuru benki hiyo kwa hatua hiyo kwa jitihada zake za kuiboresha ligi hiyo kimataifa alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha kwamba mkopo huo unarejeshwa kwa wakati huku pia akiahidi kulitunza vyema basi hilo.

“Kupitia usafiri huu sasa tuna uhakika wa kusafirisha wachezaji wote na benchi la ufundi sambamba na mashabiki zaidi kwenda kwenye mechi zetu nje ya mkoa. Tunahidi kurejesha mkopo huu ndani ya muda unaotakiwa kama tulivyokubalina na NBC’’ alisema.

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akimkabidhi ufunguo wa basi jipya Rais wa Klabu ya Singida Fountain Gate FC ya mkoani Singida Bw Japhet Makau ikiwa ni muendelezo wa sehemu ya mpango wa benki hiyo wa  utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vilabu vinavyoshiriki ligi Kuu ya Tanzania bara. Hafla ya makabidhiano ya basi hilo lenye thamani ya sh milioni 470 imefanyika jana kwenye Uwanja wa CCM Liti, Mkoani Singida ikienda sambamba na shamramshara za maadhimisho ya siku ya Singida Big Day zilizofanyika viwanjani hapo.

Rais wa Klabu ya Singida Fountain Gate FC ya mkoani Singida Bw Japhet Makau (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa basi jipya la klabu hiyo lilitolewa na Benki ya NBC  ikiwa ni muendelezo wa sehemu ya mpango wa benki hiyo wa  utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vilabu vinavyoshiriki ligi Kuu ya Tanzania bara. Hafla ya makabidhiano ya basi hilo lenye thamani ya sh milioni 470 imefanyika jana kwenye Uwanja wa CCM Liti, Mkoani Singida ikienda sambamba na shamramshara za maadhimisho ya siku ya Singida Big Day zilizofanyika viwanjani hapo

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (katikati) akizungumza wakati wa makabidhiano hayo. Wengine ni viongozi waandamizi kutoka benki hiyo pamoja na Klabu ya Singida Fountain Gate FC.

Baadhi ya viongozi wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (wa nne kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Klabu ya Singida Fountain Gate FC wakiongozwa na Rais wa Klabu hiyo Bw Japhet Makau (wa pili kulia) wakati wa hafla hiyo.

Wafanyakazi wa Benki ya NBC wakiwa kwenye picha pamoja na basi lilitolewa na benki hiyo kwa Klabu ya Singida Fountain Gate FC ikiwa ni muendelezo wa sehemu ya mpango wa benki hiyo wa  utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vilabu vinavyoshiriki ligi Kuu ya Tanzania bara.

Brand new! Muonekano wa ndani wa basi hilo.


Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC pamoja na maofisa wa Klabu ya Singida Fountain Gate FC wakiwa kwenye hafla hiyo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments