WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk, Ashatu Kijaji amesema hayupo tayari kuwakwamisha wafanyabiashara na wawekezaji kufikia malengo yao pamoja na kutatua changamoto zao ili kuhakikisha uchumi unakuwa na tija na manufaa kwa taifa .
Dk Kijaji amesema hayo alipotembelea kiwanda cha kutengeneza vishikwambi cha Tanztech kilichopo jijini Arusha kwa lengo la kujionea uzalishaji huo na kusikiliza changamoto zao.
Aidha, Dk Kijaji ameridhishwa na uwekezaji huo ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto ya matumizi ya vishkwambi katika shule za awali na zile za sekondari ambapo vitasaidia kufundisha wanafunzi namna bora ya kutumia Tehama katika mitaala ya elimu.
Mkurugenzi wa kiwanda hicho cha Tanztech , Gurveer Hans amesema kiwanda hicho kipo tayari kushirikiana na serikali katika kutoa bidhaa hiyo mashuleni na kwa watu binafsi kwa bei nafuu na kutoa ombi kwa serikali kupunguza au kuondoa ushuru wa vifaa wanavyoviagiza kutoka nje ya nchi ikiwemo VAT
Pia akiwa kiwanda cha TANFOAM kinachozalisha magodoro, Mkurugenzi Msaidizi kiwanda hicho,Meshack Jimmy ameipongeza serikali kwa jitihada mbalimbali za utatuzi wa changamoto za wafanyabiashara na wawekezaji ili kuwawekea mazingira bora ya kupata masoko ikiwemo kirahisisha ufanyaji wa biashara.
0 Comments