DK.MWINYI ASEMA MCHEZO WA NGUMI UTAFUNGUA FURSA KWA VIJANA NA KUITANGAZA ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema tarehe 27 Agosti 2023 Zanzibar imefungua ukurasa mpya wa maendeleo ya sekta ya michezo kwa kuzindua rasmi mchezo wa ngumi kuwa miongoni mwa michezo iliyoruhusiwa kuchezwa Zanzibar kama ilivyo michezo mingine kwa kuzingatia sheria na kanuni za mchezo huo kimataifa.


Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo jana usiku akizindua rasmi mchezo wa ngumi za kulipwa Zanzibar uliyoshirikisha mabondia kutoka Tanzania bara na Zanzibar uliofanyika uwanja wa Mao Tse Tung, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa uamuzi wa Serikali kuruhusu mchezo wa ngumi Zanzibar umetokana na maoni ya wananchi wengi kutaka mchezo huo uruhusiwe. Amesema haikuwa kazi nyepesi kuurudisha mchezo huo baada ya kuzuiwa kwa zaidi ya miaka 50.

Vilevile, mchezo wa ngumi ni fursa nyengine ya vijana wa Zanzibar kunufaika katika sekta ya michezo na kuweza kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya mchezo wa ngumi .

Kwa upande mwingine mchezo huo utaweza kuitangaza Zanzibar na kuchochea utalii kupitia sekta ya michezo.
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments