TIMU za kata ya Ilemela, Pasiansi, Buswelu zimepata ushindi katika michezo yao iliyochezwa jana ya mashindano ya Angeline Jimbo cup yanayoendela Wilaya ya Ilemela Mwanza.
Ilemela imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Buzuruga mchezo uliochezwa uwanja wa Sabasaba.
Pasiansi imeshinda mabao 3-1 dhidi ya Ibungiro katika mchezo uliochezwa uwanja wa Baptist.
Kata ya Buswelu imeshinda mabao 4-1 dhidi ya Nyamhongolo mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Buswelu Sekondari.
Timu ya Kayenze imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Bugogwa katika uwanja wa shule ya msingi Bugogwa. Bao la Bugogwa lilifungwa na Elias Manyama dakika ya 5 na Sila Mipawa akaisawazishia Kayenze katika dakika ya 75.
0 Comments