KAMATI YAIPONGEZA LATRA TIKETI MTANDAO

 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Miraji Mtaturu ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa kusimamia mfumo wa tiketi mtandao kwani umepunguza kero kwa abiria wa usafiri wa ardhini nchini.

Akizungumza jijini Dodoma wakati Kamati hiyo ikipokea taarifa ya Utendaji ya Mamlaka hiyo Mhe. Mtaturu amesema miongoni mwa faida za mfumo huo ni pamoja na kupunguza mianya ya uvujaji wa mapato kwani abiria ana uhuru wa kukata tiketi na hali hiyo kuruhusu mmiliki kuona idadi ya siti zilizokatwa.

“Nawapongeza sana LATRA sababu kupitia mfumo wa tiketi mtandao sasa hivi abiria anaweza kukata tiketi akiwa popote bila kulanguliwa na maajenti, lakini mfumo huu umerahisisha ukusanyaji wa mapato kwa wamiliki na Serikali sababu unaweza kuona idadi za tiketi moja kwa moja kupitia mfumo’’ amesema Mhe. Mtaturu.

Aidha, Mhe. Mtaturu ameitaka LATRA kuhakikisha Kampuni ya Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) zinaharakisha kuingia kwenye mfumo wa   tiketi mtandao ili kuwarahisishia abiria kwani wamekuwa wakitumia muda mrefu kupanga mistari katika stesheni ili kupata tiketi.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta a Ujenzi), Mhe. Atupele Mwakibete amesema Serikali imeanza kutekeleza mkakati madhubuti wa kudhibiti ajali kwa kufanya utafiti kupitia gari maalum likalobainisha maeneo yenye changamoto za ajali ili kuja na suluhu itakayosaidia kuondoa ajali zinazosababishwa na ubovu wa barabara.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habib Suluo ameihakikishia Kamati kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu na kufanyia kazi ushauri uliotolewa kwa lengo la kuboresha shughuli za usafirishaji ikiwemo kuendelea kuwatahini madereva ili kuhakikisha abiria wanasafiri kwa usalama.

 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Miraji Mtaturu akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete  na Wataalam wa Wizara (hawapo pichani), wakati kamati hiyo ilipopokea taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Bungeni jijini Dodoma. 

 Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Mhe. Atupele Mwakibete akiwasilisha taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani), Bungeni jijini Dodoma. 

 Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Atupele Mwakibete akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo wakati wa kuwasilisha taarifa ya utendaji wa Mamlaka hiyo kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundomboinu, Mhe. Ghati Chomeke akisisitiza jambo, wakati  Kamati hiyo ilipopokea taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Bungeni jijini Dodoma leo.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo akifafanua jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani), kuhusu shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati alipowasilisha taarifa ya utendaji, Bungeni jijini Dodoma leo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments