KATAMBI: RAIS SAMIA AMELETA NAFUU KWA WAWEKEZAJI KUONDOA TOZO ZA OSHA

RAIS Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwathamini wawekezaji kwa kuridhia kupunguzwa na kufutwa baadhi ya tozo zilizokuwa zikitozwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) zenye thamani ya Sh.Bilioni 35.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameyasema hayo leo Agosti 18, 2023 jijini Dodoma kwenye kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya OSHA.

Alisema hatua hiyo ilitokana na ombi la wafanyabiashara kupitia Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) ili kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji nchini.

Katambi alisema masuala ya usalama na afya mahali pa kazi yataendelea kupewa uzito na serikali ili kuhakikisha nguvu kazi iliyopo inakuwa salama.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq alipongeza serikali kwa kuendelea kufanyia kazi maoni ya kamati ya kuimarisha masuala ya usalama mahali pa kazi kwa kuipatia OSHA vitendea kazi ili itekeleze majuku yake kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, alisema tozo ya upimaji umeme katika vituo vya mafuta hasa maeneo ya vijijini imepunguzwa kutoka Sh.650,000 hadi Sh.150,000 ili kuvutia wawekezaji na kuondokana na mafuta kuuzwa kwenye chupa.

Alisema kumekuwapo na matokeo chanja ambapo OSHA imevifikia vituo 2,708 ikilinganishwa na kabla ya kupunguzwa tozo vilifikiwa vituo 1,153.

Kadhalika, alisema kutokana na Tanzania kutekeleza kwa kiwango kikubwa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi imekuwa mfano kwa mataifa mengine kuja kujifunza.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akifafanua jambo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 18 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya OSHA, kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, tarehe 18 Agosti, 2023, jijini Dodoma.Baadhi ya Wajumbe Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya OSHA, Bungeni, tarehe 18 Agosti, 2023, jijini Dodoma.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Mendeleo ya Jamii Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akizungumza jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya OSHA, leo tarehe 18 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa kamati hiyo Bi. Aziza Kheir.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Boniphace Getere akichangia jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya OSHA, leo tarehe 18 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma.


Baadhi ya Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakifuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, tarehe 18 Agosti, 2023, jijini Dodoma.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments