Mavunde kuwanoa walimu wa Sayansi Dom

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma,  Anthony Mavunde anatarajia kuandaa mafunzo maalum kwa walimu wa Sayansi na Mafundi sanifu wa Maabara za Shule za Sekondari  Jijini Dodoma.
 Lengo la mafunzo hayo ni  kuwajengea uwezo na maarifa zaidi katika matumizi ya vifaa vya maabara.
Mavunde ameyasema  hayo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Bunge iliyopo Kikombo,Dodoma wakati akikabidhi seti ya Televisheni na King’amuzi cha DSTV kwa ajili ya matumizi ya shule ikiwa ni utekelezaji wake wa ahadi aliyoitoa wakati wa mahafali ya Pili ya Kidato cha Sita shuleni hapo.
“ Tunawashukuru wabunge kwa mchango wao mkubwa kwenye sekta ya elimu uliowezeshwa kujengwa kwa shule hii ya wasichana ya mchepuo wa Sayansi.” Amesema na kuongeza
” Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya zaidi ya sh bilioni 2 katika kuiboresha shule hii.” Amesema Mavunde.
Nae, Diwani wa Kata ya Kikombo  Emmanuel Manyono,  na Diwani Viti Maalum Wendo Kutusha na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Fred Mushi wamemshukuru Mavunde kwa kuwajali wanafunzi na kutimiza ahadi yake kwa Shule ya Sekondari Bunge.
Akitoa taarifa ya awali,Mkuu wa Shule ya Sekondari Bunge, Salome Mkombola amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha shule hiyo inafanya vizuri kwenye taaluma kwa kuzalisha wanasayansi wengi wa kike wenye uadilifu na nidhamu kubwa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments