Mbunge ateuliwa kugombea ubunge Mbarali

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua, Bahati Ndingo kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mdogo jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.

Kwa sasa Bahati ni Mbunge wa Viti Maalum CCM, kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi huo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Francis Mtega aliyefariki Julai Mosi kwa ajili ya pikipiki na gari jimboni humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa  Agosti 17 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema uteuzi huo umefanywa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.

“Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Bahati Keneth Ndingo kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya,” imesema sehemu ya taarifa iliyotolewa na chama hicho.

Bahati ameteuliwa kufuatia ushindi alioupata katika kura za maoni katika jimbo hilo, akiongoza watia nia 25 waliogombea.

Mbali na jimbo la Mbarali, NEC ilitangaza uchaguzi mdogo wa udiwani kufanyika katika kata sita kutoka Halimshauri nne nchini.

Kata hizo ni pamoja na Nala (Halmashauli ya Jiji Dodoma), Mfaranyaki (Manispaa ya Songea), Mtyangimbole (Madaba), Old Moshi Magharibi (Moshi), Marangu Kitowo (Rombo).

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments