Mbunge wa Same ataka kauli kutuama maji barabara Dar

Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Malecela, amehoji kauli ya Serikali kuhusu kadhia ya maji yanayotuama maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na hasa wakati wa mvua.

Akijibu swali hilo leo Jumatatu 29, 2023, Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Festo Dugange amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti athari zinazotokana na mvua katika jiji hilo.

Amesema hatua hizo ni pamoja na kujenga kingo za mito na mifereji mikubwa yenye urefu wa kilomita 30.7 kwa thamani ya Sh60 bilioni kupitia mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP).


Amesema kupitia mradi wa DMDP awamu ya pili, Serikali inafanya usanifu na utambuzi wa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa mifereji na mito yenye urefu wa kilomita 101.15 inayokadiriwa kutumia Sh200 bilioni katika wilaya zote za Mkoa Dar es Salaam.

Amesema Wakala wa Barabara za Vijini na Mijini (Tarura), kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), wanaendelea na ukamilishaji wa kazi ya ununuzi, kwa ajili ya uboreshaji wa mto Msimbazi ikiwa ni jitihada za Serikali kuendelea kukabiliana na mafuriko katika Jiji la Dar es Salaam.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments