“Miradi ibebe dhana ya maendeleo”

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Abdalla Shaib Kaim ametaka utekelezaji wa miradi inayopitiwa na mwenge huo ibebe dhana na maono kwa kuleta maendeleo chanya kwa wananchi.

Shaib alisema hayo wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita, kukagua, kutembelea na kuweka Jiwe la Msingi katika miradi mbalimbali kwenye Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Amesema ni lazima utekelezaji wa miradi inayopitiwa na mwenge wa uhuru ilete maendeleo na mabadiliko yanayoonekana kwa wananchi.

Akiwa katika halmashauri hiyo kiongozi huyo amewajia juu viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kuhakikisha wanaweka vizuri taarifa zao za utekelezaji wa miradi ili kuwezesha ukaguzi kuwa rahisi kwani mpangilio mbaya wa nyaraka unalenga kuficha nia ovu ya watendaji wa halmashauri katika usimamizi wa fedha za miradi hiyo.

Kaim alisema kuwa mbio za mwenge za mwaka huu jambo hilo limemkwamisha kufanya ukaguzi wa taarifa za fedha na utekelezaji wa miradi kwenye halmashauri hiyo na hivyo kutoa maelekezo kwamba pamoja na kupitishwa kwa miradi 12 iliyopitiwa na mwenge ametoa siku nne nyaraka ziwekwe vizuri kwa maelekezo aliyotoa na zimfikie popote atakapokuwa.

Hata hivyo kiongozi huyo ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya barabara,maji, madarasa na fedha za mikopo kwa makundi maalum huku akitoa wito kwa halmashauri kutekeleza miradi kwa wakati ili kuwezesha wananchi kupata huduma.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ambayo itapitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mwantumu Mgonja alisema kuwa miradi 12 yenye thamani ya Sh bilioni 3.1 ilitarajia kupitiwa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments