MTATURU AKOSHWA NA MAENDELEO KATA YA KIKIO

 

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekabidhi vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya Sh Milioni 5 katika shule ya Sekondari ya Mkunguwakihendo ikiwa ni jitihada zake za kuunga mkono kampeni ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya Tanzania ya kidigitali.

Mtaturu amekabidhi vifaa hivyo Agosti 6,2023, akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake katika Kata ya Kikio ya kutembelea miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi pamoja na kurudisha mrejesho wa shughuli za bunge la bajeti.

"Tunafahamu namna ambavyo serikali yetu inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili yetu,na sisi kama wabunge ni jukumu letu kuunga mkono jitihada hizi serikali,"amesema.

Aidha mbunge Mtaturu ametembelea kitongoji cha Mwitumi ambacho wanajenga shule shikizi ambapo watoto wanatembea km 10 kila siku kufuata shule ya msingi Nkundi huku wakivuka mito miwili mikubwa kufanya kipindi cha masika kukosa shule na utoro wa rejereja.

Ili kuondokana na changamoto huyo Mtaturu aliwachangia Sh Milioni 2 ambapo kwa sasa ujenzi wa madarasa mawili na ofisi umefika kwenye lenta.

Aidha kupitia ziara hiyo amewaongeza Sh Milioni 10 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nkundi Getruda Ghamaa amemshukuru mbunge kwa maendeleo mbalimbali anayowapelekea katika sekta za Elimu na Umeme ikiwemo michango hiyo ya kumalizia madarasa ya shule shikizi ya Kitongoji cha Mwitumi ambayo ni changamoto kubwa kwa wanafunzi.


      

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments