Mwenge wa Uhuru kupitia miradi ya Sh bilioni 29 Geita

MBIO za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 zimewasili mkoani Geita kutokea mkoani Shinyanga ambapo utakimbizwa katika halmashauri sita, kutembelea, kukagua na kuzindua miradi 59 yenye thamani ya Sh bilioni 29.

Akizungumuza leo wakati wa mapokezi ya mwenge katika kijiji cha Nyang’olongo wilayani Nyang’hwale, Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigela alisema Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani hapa utakimbizwa Km 755.54.

Amefafanua, viongozi wa mbio za mwenge wanatarajia kufungua miradi mitatu, kuzindua miradi 21, kukagua miradi 22 na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 13.

Amesema kwa kuzingatia ujumbe wa mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2023, usemao Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai na kwa Ustawi wa Uchumi mkoa umetekeleza miradi tofauti ikiwemo upandaji miti.

Shigela amesema kwa mwaka 2022/23 mkoa umepanda jumla ya miti milioni 5.07, uhamasishaji wa matumizi ya nishati mbadala kwa taasisi na wananchi na utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya usafi mwisho wa mwezi.

Amesema pia mkoa unaendelea kuunga mkono juhudi za kitaifa za kupamabana na maambukizi ya viruisi vya ukiwmi ambapoo mkoa umepunguza Kasi ya maambukizi ya hadi kufikia asilimia tano kwa utafiti wa mwaka 2016).

Amesema pia takwimu za upimaji zinaonesha kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 waliopimwa UKIMWI katika Mkoa wa Geita ni watu 436,031.

“Kati ya hao wanaume ni 147,825 na wanawake ni 288,206 huku wananchi waliokutwa na maambukizi ni 11,926 kati yao wanaume 4,662 na wanawake ni 7,264 sawa na asilimia 2.7.” Ameeleza Shigela.”

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023, Abdullah Shaibu Karimu amesisitiza watapitia miradi husika kujiridhisha ubora na thamani halisi ya miradi na utekelezaji wa kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments