Rais Samia Atembelea Ujenzi Wa Kituo Cha Afya Kizimkazi Kinachojengwa Kwa Ushirikiano Wa Serikali Na Benki Ya NBC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ametembelea ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ikiwa ni jitihada za wadau hao wawili katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.

Ziara ya Rais Samia kwenye eneo hilo la mradi imefanyika jana ikiwa pia ni sehemu ya ufungaji wa Tamasha la Kizimkazi 2023. Katika Ziara hiyo Rais Samia aliambatana na viongozi waandamizi kutoka serikalini na Chama tawala cha CCM akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi, viongozi waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi pamoja na wakazi wa eneo hilo.

Akizungumzia mradi huo wenye thamani ya sh bilioni 4.4 ambapo benki ya NBC imechangia kiasi cha Sh milioni 400, Rais Samia pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa hatua hiyo muhimu, alisema huo ni adhma ya serikali kuboresha huduma ya afya kwa kujenga vituo vya afya kwenye maeneo mbalimbali kulingana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo katika maeneo hayo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi (alieshika kipaza sauti) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa benki hiyo kwenye ujenzi wa mradi wa kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakati Rais alipotembelea mradi huo jana ikiwa pia ni sehemu ya ufungaji wa tamasha la Kizimkazi 2023. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi (wa pili kulia).



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan (katikati) akimsikiliza Mhandisi wa mradi Mhandisi Fatma Kara (alieshika kipaza sauti) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakati Rais alipotembelea mradi huo jana ikiwa pia ni sehemu ya ufungaji wa tamasha la Kizimkazi 2023. Wengine ni pamoja na viongozi waandamizi wa serikali, Chama tawala na benki hiyo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi (wa tatu kulia) wakati wa hafla hiyo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Zanzibar Ramadhan Lesso (wa tatu kushoto) wakati akielezea huduma zinazotolewa na benki hiyo wakati Rais alipotembelea banda la benki ya NBC lililopo kwenye eneo la Tamasha la Kizimkazi 2023 Paje, Mkoa wa Kusini, Unguja.


Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi ( wa nne kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Benki ya CRDB akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa (wa tatu kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo Uhusiano wa NBC, Godwin Semunyu (kushoto) na Meneja Mawasiliano wa benki ya NBC Brendansia Kileo (Kulia)


Kata simu NBC tuko site! Ndivyo anavyosika Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi akiongea na simu wakati akikagua ujenzi wa mradi wa kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na benki hiyo.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa mradi wa kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na benki ya NBC.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments