MASHINDANO ya Angeline Jimbo cup yanatarajiwa kuendelea Septemba 4, 2023 kwa mchezo mmoja wa robo fainali utakaozikutanisha timu za kata ya Ilemela dhidi ya Ibungiro.
Mchezo huo na mengine yote ya robo fainali inatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa shule ya msingi Sabasaba wilayani Ilemela.
Mchezo mwingine utacheza Septemba 5 kati ya kata ya Sangabuye dhidi ya Nyakato.
Septemba 6 kata ya Kirumba itacheza dhidi ya Nyasaka huku Septemba 7, Shibula itacheza dhidi ya Mecco.
Naye katibu wa mbunge wa jimbo la Ilemela, Charles David amezipongeza kata zote nane kwa kufuzu hatua ya robo fainali.
Ameziomba timu hizo zifike kwa wakati ili mechi za robo fainali ziwe zinaanza kwa muda uliopangwa ambao ni saa 10 kamili alasiri.
Katibu mkuu wa chama cha soka wilaya ya Ilemela(IDFA) Almas Moshi amesema timu zitakazofuzu hatua ya nusu fainali zitapewa jezi.
0 Comments