Samia: Hakuna mwenye ubavu kuligawa Taifa

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa ameamua kunyamaza kimya na ataendelea kunyamaza kimya, lakini hakuna mwenye misuli na ubavu  wa kuligawa Taifa wala kuuza Taifa ,au kuharibu amani na usalama  wa nchi.

Rais Samia amesema hayo wilayani Arumeru mkoani Arusha kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu mkoani Arusha Agosti 21, 2023.

Amesema amesikia yote aliyosema Askofu Dk, Fredrick Shoo kuhusu usalama,amani,umoja wa Taifa. “Nimeyasikia yote ,niliamua kunyamaza kimya na nitaendelea kunyamaza kimya,na hakuna mtu mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama uliojengwa katika Taifa hili na haya itoshe kuwa ni ujumbe wangu kwenu,” amesema Rais Samia.

Naye  Dk Shoo amemuomba Rais Samia kufanya kazi zake kwa kujiamini na ujasiri, kwani Mungu ndiye aliyemuweka na kusisitiza kuwa kanisa hilo linaunga mkono uwekezaji wa suala la bandari.

Amesema kuna watu hawamuamini na hawakutaka  kuona mwanamke akiongoza, lakini afanye kazi zake kwa kujiamini na ujasiri, kwani Mungu ndiye  amemuweka katika nafasi hiyo na hilo ndilo wanalolisheshimu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments