Sita kuwania mchezaji bora EPL

ERLING Haaland ni mmoja wa wachezaji watatu wa Manchester City walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha soka FA.

Mshambuliaji huyo raia wa Norway mwenye umri wa miaka 23 alifanya makubwa katika msimu wake wa kwanza England.

Alifunga mabao 52 katika michuano yote huku vijana wa Pep Guardiola wakishinda Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA.

Katika orodha hiyo ya wachezaji sita wamejumuishwa ne Kevin De Bruyne na John Stones.

Wachezaji wawili wa Arsenal Bukayo Saka na Martin Odegaard pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Spurs Harry Kane, ambaye sasa yuko na Bayern Munich, wanakamilisha orodha hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments