TASAC yaiomba serikali kutatua changamoto ziwa Rwakajunju

KAGERA: Bodi ya Shirika la Uwakala wa meli Tanzania TASAC Imetoa wito kwa serikali ya mkoa wa Kagera kuhakikisha wanaandaa Mazingira mazuri kwa vijana wanaotumia Ziwa Rwakajunju wilayani Karagwe na kwenda nchini Rwanda kwa ajili ya kuuza bidhaa zao huku wakikabiliwa na changamoto ya kutobeba bidhaa yeyote kutoka Rwanda kuja kuuza Tanzania.

Tathimini ya Bodi hiyo kupitia ziara iliyofanyika Mkoani Kagera kwa muda wa siku 5 katika kuhakikisha wanakagua maeneo wanavyofanya nayo kazi na kutoa maelekezo pamoja na kubaini changamoto mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha ,Mussa Hamza Mandia amesema kuwa Kuna changamoto kadhaa ikiwemo vijana wanaotumia Ziwa Rwakajunju lililopo katika mpaka wa Karagwe na Rwanda wanapoleta bidhaa kutoka Rwanda inachukuliwa Kama Magendo.

Amesema vijana wengi wanaenda kuuza bidhaa zao Rwanda wakifika Rwanda wanalipwa Faranga na wakifika katika wilaya ya Karagwe wanashindwa kubadilisha fedha hizo ,na ikitokea wakasema wanunue bidhaa waje kuuza mkoani Kagera wanakamatwa na mamlaka mbalimbali na kuchukuliwa hatua Kali Jambo ambalo amesema linawanyima Fursa na wanakosa kukuza uchumi wao.

“Serikali iangalie pale ,mkoa wa Kagera unapoteza pesa ,mapato na kila kitu kwanza Hakuna sehemu ya kubadili hizo fedha za Rwanda wanahangaika,Pili wanachukuliwa Kama wahalifu kila wakijaribu kununua bidhaa Rwanda na kuileta Tanzania, je Kuna maaana gani ya kuwa na jumuiya Moja Kama hamuwezi kubadilishana uzoefu wa kibiashara na bidhaa ?? serikali lazima itupie jicho pale hiyo ni changamoto “alisema Mandia

Alisema changamoto nyingine ambayo imebainika kupitia kamati hiyo Ni matumizi makubwa ya vifaa vya Solar Kama zana ya kutegea samaki huku Mamlaka zikijua kuwa zana hiyo inachangia kuharibu mazalia ya samaki ambapo alisema kuwa bodi itafikisha maombi serikalini ya kupiga marufuku vifaa vinavyoharibu mazalia ya samaki ili kulinda Rasilimali za ziwa Victoria .

Ameongeza  kuwa changamoto nyingine ni wavuvi kutojua mipaka kati ya mpaka wa ziwa Victoria upande wa Tanzania na Uganda Jambo ambalo linazua migogoro ya Mara kwa Mara huku akitoa wito kwa mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwasa kuhakikisha wanafanya haraka vikao vya ujirani mwema ili kunusuru wavuvi hao pale wanapokuwa wamevuka mipaka.

Aidha bodi hiyo imeuomba uongozi wa mkoa wa Kagera kuanzisha vizimba vya kuzalisha samaki ili kuongeza uchumi wa wakazi wa mkoa wa Kagera pamoja na kujenga barabara nzuri inayoelekea katika mwalo wa Magarini.

Hata hivyo alisema pamoja na changamoto hizo ndondogo bado serikali imeshughulikia changamoto nyingi ikiwemo uboreshaji wa mipaka,ujenzi wa Miundo mbinu ,uimarishaji wa usalama katika visiwa vya ziwa Victoria pamoja na ukarabati unaoendelea wa kukarabati kivuko Cha Kyenyabasa kinachowavusha wananchi wa Bukoba vijijini.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments