BAADA ya kukamilisha taratibu zote, ikiwemo vipimo vya afya na kusaini mkataba, Manchester United imepanga kumtambulisha Rasmus Højlund kuwa mshambuliaji mpya kesho.
Hojlund utaongeza upana eneo la mwisho, ambalo mara kadhaa kocha Eric Ten Hag amekuwa akimtumia Anthony Martial na Marcus Rashford ambao sio namba tisa asilia.
Mkali huyo wa mabao raia wa Denmark, licha ya uwezo wake wa kufungwa kwa mguu wa kushoto, pia ana uwezo wa kushuka chini kusaka mpira, na kuanzisha mashambulizi akiwa kwenye eneo la tatu.
Msimu ulioisha wa Seria A, Hojlund alimaliza akiwa na mabao 9 na pasi za mabao 2 katika michezo 32 aliyocheza akiwa Atalanta.
Akiwa na Sturm Graz ya Austria msimu wa 2021/2022, Hojlund alifunga mabao tisa katika michezo 18.
0 Comments