UTEUZI: RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuhamisha aliyekuwa Waziri wa Nishati, Januari Makamba kutoka wizara hiyo na kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Taarifa iliyotolewa leo kutoka Ikulu imeeleza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje ni Stephen Byabato ambaye hapo awali alikuwa ni Naibu Waziri wa Nishati.

Aidha Rais Samia amemhamisha Balozi Pindi Chana kutoka kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Wizara ya Nishati. Awali alikuwa Waziri wa Madini.

Katika taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Dk Moses Kasiluka imeeleza Rais Samia amemteua Anthony Mavunde kuwa Waziri wa Madini, awali alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi.

Makame Mbarawa ameteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi, awali alikuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.

Rais Samia pia amemuhamisha Waziri Innocent Bashungwa kutoka kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na kuwa Waziri wa Ujenzi.

Stergomena Tax amehamishwa kutoka kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Aidha, Mohammed Mchengerwa amehamishwa kutoka kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii na kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi.

Soma zaidi kupitia taarifa ya Ikulu…..

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments