Wadau maendeleo ya vijana kukutana Dar

WADAU wenye dhamana ya kupigania maendeleo ya vijana nchini wanakutana kesho jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uwezeshaji kiuchumi wa kundi hilo.

Mratibu wa programu ya AHADI katika Taasisi ya Biashara Kibaha, Prof Lemayon Melyoki amebainisha hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mpango wa AHADI unatekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania kupitia mfumo inayotokana na ushahidi ikiwa ni pamoja na vikundi vya Care na klabu za IMPACT Plus, ili kuongeza kasi kwa njia ya elimu kwa makundi ya vijana rika katika mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam, ili kuongeza uelewa juu ya masuala ya afya ya uzazi na haki za ngono (SRHR) miongoni mwa mambo mengine.

Alisema, mkutano huo unalenga kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana wenye umri wa kati ya miaka 15-19 utakaobainisha masuala yanayohusu uhuru wao wa kifedha.

“Utafiti uliofanywa na Shirika la World Vision jijini Dar es Salaam na Dodoma ulibaini kuwa vijana wengi, hususan wasichana, wanakabiliwa na changamoto kama vile mimba za utotoni kutokana na umaskini katika familia zao, na hivyo kuishia kuingia kwenye mitego ya watu wenye nia ovu ili kutimiza matakwa yao, ” amebainisha Prof Melyoki.

Amesema mkutano utavutia ushiriki kutoka kwa serikali, Asasi za Kiraia (AZAKI), vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na miongoni mwa wengine wanaohusika katika kusaidia afua za vijana.

Prof Melyoki amesema miongoni mwa mada ni pamoja na ushirikishwaji wa vijana katika uundaji wa sera, kuwatambulisha katika fursa zilizopo za uwezeshaji pamoja na kuwajengea uwezo na ujuzi wa kupata ajira au kujiajiri.

Amebainisha kuwa lengo kuu ni kuwezesha kundi hilo kupata uhuru wa kifedha katika kuendesha maisha yao ya kila siku badala ya kujihusisha na tabia zisizofaa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments