Wanawake Pwani wanavyonufaika na kilimo cha nazi

WAKINAMAMA mbalimbali kutoka Mkoa wa Pwani wamekuwa wakinufaika na kilimo cha nazi baada ya wawekezaji wengi kuwekeza katika bidhaa hiyo na kufanya kilimo hicho kupanda thamani.

Akizungumza na HabariLEO, mfanyabiashara wa kuuza na kubangua nazi, Khadija Mohamed amesema zao hilo limekuwa likipata umaarufu kutokana na watu wengi kutumia mafuta ya nazi kujipakaa.

Alimshukuru Mkurugenzi wa Active Mama, Ernestina Mwenda ‘Cocunut Lady’ kutokana na kuwaunga mkono kwa kununua nazi nyingi  ambazo zinawasaidia katika kujikimu.

Alisema kampuni ya Active Mama imekuwa mstari wambele katika kuhakikisha inasaidia wakinamamawengi kwa kununua nazi katika maeneo yao nakufanya ubanguaji wa nazi hali ambayo inafanyainawapa ajira mara mbili.

“Kwanza tunauza nazi ambapo tumekuwa tukipatafedha za kutoshalakini pia amekuwa akibangua nazina kufanya tupate ajira nyingine” alisema Khadija.

Ernestina alisema amekuwa akitumia nazi za asilikatika kutengeneza mafuta ya Active Mama, ikiwakama sehemu ya kuunga mkono kilimo cha nazi lakinipia kuifanya jamii kutotumia kemikali katika miili yao.

Unapotumia mafuta ya nazi ya asiliunafanya ngoziyako ibaki katika ubora unaostahililakini piaunasaidia kilimo cha nazi kwa ndani ya nchi.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments