WAAJIRI katika sekta rasmi na zisizo rasmi wamehimizwa kutenga sehemu maalum kwaajili ya wafanyakazi wanawake wanaonyonyesha ili waendelee kufanya hivyo wakiwa kazini.
Takwimu zinaonesha kuwa idadai ya watoto wanaonyonyesha maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita imeongezeka kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi asilimia 64 mwaka 2022.
Pia takwimu za watoto wanaonyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa imeongezeka kutoka asilimia 53.5 mwaka 2018 hadi asilimia 70 mwaka 2022.
Naibu waziri wa Afya ,Dk Godwin Mollel amesema miongoni mwa changamoto zinazokabili haki ya uzazi kwa wanawake ni uelewa duni wa baadhi ya waajiri ,wafanyakazi na jamii kuhusu jambo hilo.
“Changamoto zingine ni ukiukwaji wa haki ya uzazi za wanawake wanaofanya kazi katika baadhi ya sekta rasmi na sekta zisizo rasmi ambayo inatokana na kukosekana kwa mazingira wezeshi katika mifumo ya kijamii ya kuwasaidia wanawake waweze kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo.
0 Comments