AGRI THAMANI, FAO YAWAKUTANISHA VIJANA PAMOJA NA WATUNGA SERA KUJADILI CHANGAMOTO KWENYE MIFUMO YA CHAKULA

 

TAASISI ya Agri Thamani na Shirika la Chakula Duniani (FAO) wameandaa forum ya vijana ili kuweka mikakati na kujadili changamoto za kisera kwenye Mifumo ya Chakula na Kilimo Tanzania.

Hii inaenda sambamba na uzinduzi wa WFF chapter ya Tanzania ambayo itaenda kuchochea mabadiliko ya Sera na mifumo, WFF chapter ya Tanzania itaendeshwa na Agri Thamani.

Akizungumza katika hafla hiyo ambayo imefanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Agri Thamani Mhe. Neema Lugangira amesema vijana wamekuwa wakilalamika hawapati fursa ya kukutana na viongozi hivyo Agri Thamani wamewakutanisha wabunge toka nchi mbalimbali ambapo vijana wanatakiwa kutumia fursa hiyo kuuliza maswali na kujifunza.

Kwa upande wa vijana walioshiriki hafla hiyo wamesema kwa upande wa vijana wakulima wanapata changamoto kubwa ya ardhi, rasilimali fedha ambapo zingeweza kuwasaidia kuwasogeza katika hatua nzuri kimaendeleo.

"Rasilima Fedha kwetu ni changamoto kubwa sana, tunapohitaji mikopo marejesho yanaanza mapema sana, tunahitaji muda zaidi kabla ya rejesho". Amesema mmoja wa vijana walioshiriki hafla hiyo.

Kwa upande wa mmoja wa wabunge kutoka nchini Malawi amewaomba vijana wasiogope kushiriki katika kilimo na zaidi wafanye tafiti na wajenge urafiki na wazee waliofanikiwa katika kilimo ili wawape muongozo.

"Kwa sasa dunia ni kama kijiji ni vyema mkaangalia yanayofanya vizuri kwenye nchi zingine na kuyachukua hapa. Africa inaweza kulisha Africa na Dunia Kwa ujumla". Amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

POST A COMMENT

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments