Baleke apiga tatu

MSHAMBUIAJI wa Simba SC, Jean Baleke amekuwa mchezaji wa pili Ligi Kuu, kufunga mabao matatu ‘hat-trick’ katika msimu mpya wa ligi hiyo.

Baleke amefanya hivyo katika mchezo unaoendelea muda huu ambapo Simba inaongoza mabao 3-0 dhidi ya Coast Union.

Mchezaji wa kwanza kufanya alikuwa Feisal Salum wa Azam FC aliyefunga mabao matatu katika mchezo dhidi ya Kitayose FC.

Post a Comment

0 Comments