Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 8, 2023 mara baada ya kukabidhiwa trekta moja na kampuni ya John Deere katika jukwaa la mifumo ya chakula la Afrika (AGRF) linalofungwa leo katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Trekta ambayo Kampuni ya John Deere imeikabidhi serikali leo Agosti 08, 2023 ili kukuza Kilimo hapa nchini.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI imesema inahitaji kiasi cha shilingi bilioni 650 ili kuwekeza zaidi katika kupata mbegu bora za mazao yote zilizofanyiwa tafiti kwaajili ya kilimo hapa nchini.
Hayo ameyasema waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 8, 2023 mara baada ya kukabidhiwa trekta moja na kampuni ya John Deere katika jukwaa la mifumo ya chakula la Afrika (AGRF) linalofungwa leo katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa (JNICC) jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa 2021 Tanzania ilikuwa inauwezo wa kuzalisha asilimia 20 tu ya mbegu za mazao yote.
Amesema kwa sasa Tanzania nauwezo wa kuzalisha mbegu kwa asilimia 50 ya uzalishaji wa mbegu za mazao yote nchini lakini inaendelea kuwekeza kwenye mashamba umma kwajili ya uzalishaji wa mbegu.
Waziri Bashe amesema mwaka jana 2022 miundombinu ya umwagiliaji imeanza kujengwa kwaaajili ya kulima mbegu zinazokidhi vigezo hapa nchini.
"Makadirio ya mahitaji kwenye kilimo ni makubwa, lakini mahitaji halisi ni tani 120,000 ya mbegu za mazao yote." Amesema Bashe
Mwelekeo wa serikali na maelekezo ya Rais ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alisema kufikia mwaka 2025 Tanzania izalishe asilimia 75 ya mbegu bora za mazao ya chakula ziweze kuzalishwa ndani ya nchi ili kuacha kuagiza kutoka nje.
"Na sisi serikali tuweke nguvu kwenye utafiti ili tuweze kuleta mbinu bora za kilimo cha kisasa na waweze kuwapa sekta binafsi waweze kuzalisha kwa wingi." Amesema
Amesema wakulima nchini wameshaaza kuzalisha tani 60,000 ambayo ni asilimia 50, ya mahitaji na njia iliyoweza kuongeza uzalishaji ni njia mbili ambazo ni makadirio ya mahitaji na mahitaji halisi.
Amesema serikali imeandaa mashamba 17 ambayo watapewa sekta binafsi za watanzania kwaajili ya kufanya shughuli za uzalishaji mbegu bora, ambazo watanzania watahitaji katika kilimo cha kisasa.
Akizungumzia kuhusiana na trekta ambalo serikaliI imepokea amesema kuwa serikali kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya ya Mifumo ya Chakula (AGRA) itandaa shindano kwa vikundi vya vijana wanaofanya Kilimo biashara watatuma maandiko yao na atakayeshinda atapata trekta hilo.
"Kikundi kitakachoshinda kitakabidhiwa trekta na tunaangalia trekta hiyo kwa sababu Business plan itaeleza eneo litakalofanyiwa kazi ndio litakalo tafsiri vifaa vitakavyokuwepo. Ili kuangalia namna vijana watakavyoenda kufanya kilimo cha kibiashara.
Amesema serikali inatafuta mbinu za kiwaingiza vijana katika kilimo, sio kila kijana atakuwa na shamba, kunamwingine atalima, mwingine atauza mbegu mwingine atatoa huduma za ugani.
0 Comments