DKT. BITEKO:PESA ZA MAMA SAMIA NI ZA MOTO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko amewataka watendaji wa serikaki kote nchini kufanya kazi kwa weledi bidii na maarifa na kuwaeleza kuwa wasijaribu kutapanya pesa za miradi ya maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao kwani kufanya hivyo ni sawa na kuchezea moto

Dkt. Biteko ameyasema hayo aliposimamishwa na wananchi wa Sengerema na kuwasalimia akiwa njiani kuelekea Geita ambako anakwenda amezindua maonyesho ya sita ya kikataifa ya teknolojia ya madini

“Rais wetu anahangaika usiku na mchana kutafuta fedha ili zilete maendeleo na kuinua hali za wananchi wetu, Rais anatengeneza miundombinu ya barabara, miondombinu ya maji, umeme vituo vya afya nakadharika, Elimu nakadharika “.

“Nitoe wito kwa viongozi wa Serikali mlioko Sengerema, kipaumbele chetu cha huduma tumuangalie mtanzania aliye masikini, aliye kijijini tumhudumie. Huyo hana cha kufanya zaidi ya kusubiri mipango ya Serikali imuokoe kwenye shida yake, huyo anasubiri serikali imjengee barabara, huyo anasubiri zahanati ijengwe karibu yake mke wake akatibiwe karibu, huyo anasubiri mtoto wake ajengewe madarasa, kuwe na madawati kuwe na walimu huyo ni masikini huyo ndio tumuangalie” amesisitiza Dkt. Biteko

“Nataka niwaambieni kila mahali kuliko na fedha ya Serikali, sisi tupo mama hataki mchezo atakayejaribu kugusa hela ya Serikali huyo amekutana na moto wa mama” aliongeza

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments