Ligi pendwa EPL imerejea

ENGLAND: Baada ya mapumziko ya wiki moja kupisha michezo ya kimataifa, Ligi Kuu nchini England inarejea leo kwa michezo kadhaa.

Mchezo wa mapema utakuwa kati ya Liverpool dhidi ya Wolves, utapigwa saa 8:45 mchana.

Fulham dhidi ya Luton, Spurs watakuwa nyumbani kuwakaribisha Sheffield United, West Ham watakuwa London Stadium kuwakaribisha vijana wa Pep Guardiola, Man City, Man United dhidi ya Brighton, Aston Villa dhidi ya Crystal Palace, michezo yote itapigwa saa 11:00 jioni.

Newcastle United watakuwa St James Park kuwakaribisha ‘The Bees’ Brentford, mchezo huo utapigwa saa 1:30 usiku.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments