Mahakama yaamuru Bocco kulipwa Sh milioni 200

Mahakama Kuu ya Tanzania imeamuru kuwa mshambuliaji wa klabu ya soka ya Simba na Taifa Stars, John Bocco alipwe fidia ya Sh milioni 200 na kampuni ya mchezo wa kubashiri ya Princess Leisure (T) Limited, kwa kutumia picha yake kwenye tangazo lao.

Uamuzi huo umetolewa Agosti 31, 2023 na Jaji Irvin Mugeta.
Awali, Bocco aliiomba mahakama iamuru kampuni hiyo imlipe jumla ya Sh bilioni 1 kama fidia ya kutumia picha yake bila ridhaa yake pamoja na kumlipa Sh milioni 25 kama mrabaha kwa kipindi chote kilichotumika.


Katika tangazo hilo kuliandikwa “Burudani ya NBC inaendelea leo kwa mechi tatu. Kubwa ni Simba ambao watakuwa wageni wa Ruvu Shooting ya Mwanza pale CCM Kirumba. Muda wa pesa umerudi,”


Kupitia kesi hiyo, Bocco aliwakilishwa na mawakili wawili, Innocent Michael na Gadi Kabele ambao walidai kutumia picha yake hiyo ina maana mteja wao amevunja mkataba wake na Simba na klabu hiyo inakaribia kumchukulia hatua za kinidhamu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments