Majaliwa: Watumishi Halmashauri wakae vijijini

KIGOMA, Uvinza: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kama Rais Samia Suluhu Hassan anafanya ziara na kusikiliza kero za wananchi, haoni ni kwa nini watumishi wengine wa umma wanashindwa kufanya hivyo.

“Iwapo Mkuu wa nchi, Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan anaenda kote nchini na kusikiliza wananchi, je ninyi ni akina nani? Nilishasema mtenge siku tatu katika wiki mwende vijijini na kuwasikiliza wananchi,” alisema.

Ameyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Septemba 21, 2023) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nguruka, wilayani humo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments