MBUNGE MTATURU ASAIDIA MGONJWA

 


KATIBU wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Ally Juma Rehani amekabidhi kiasi cha Shilingi 150,000 kwa ajili ya matibabu ya mtoto Shedrack Yese anayetakiwa kupelekwa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya matibabu.

Kiasi hicho cha fedha amekikabidhi kwa niaba ya Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ili kumsaidia mtoto huyo anayesumbuliwa na seli mundu (Sickle Cell).

"Mhe Mbunge alipokea maombi yenu ya gharama za matibabu ya mtoto Shedrack, amewapa pole na kunituma niwaletee mchango wake wa matibabu,Mh Mbunge anamuombea matibabu mema apone kwa haraka Insha Allah, "amesema.

Hiyo ni baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbwanjiki Omari Kulungu kumpeleka mama wa mgonjwa ofisini kwa mbunge na kuomba msaada wa matibabu ya mtoto huyo.

Wakipokea msaada huo mzazi wa mtoto huyo wamemshukuru sana mbunge kwa moyo wake wa huruma na upendo kusaidia watu wenye uhitaji na kumuomba katibu awafikishie salaam kwa mbunge wao Mtaturu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments