Mbunge Salim awakatia vijana vibali vya kuuza mkaa

TANGA:Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hasham ameitoa zaidi ya sh Mil 1.6 Kwa ajili ya kulipa ada ya leseni ya uvunaji wa mazao ya misitu (Mkaa na kuni) Kwa Vikundi sita (6) ambavyo vina jumla ya vijana 35.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi risiti za malipo ya Vibali hivyo Katibu wa Mbunge Thomas Machupa amevitaka vikundi hivyo kufuata sheria za uvunaji wa mazao ya misitu ili kuepuka changamoto za kukamatwa mara kwa mara.

Pia amewataka vijana kutumia fursa hiyo vyema ili kujiinua kiuchumi kwani nia ya mbunge ni kuona vijana wanaojiajiri wanainuka kiuchumi ikiwa ndio njia mbadala ya kupambana na Changamoto ya ajira.

Nao wawakilishi wa vikundi hivyo wamemshukuru Mbunge Salim Alaudin kwa kutimizia ahadi na kusema wataitumia vyema fursa hio kukuza vipato vyao na familia zao ili kuondokana na umaskini.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments