Mikakati yawekwa mafuta ya kula

 

SERIKALI imesema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kutekeleza mkakati wa kuendeleza sekta ndogo ya alizeti na chikichi ambayo ndiyo mazao makubwa yanayoweza kuzalisha kwa tija mafuta ya kupikia nchini kwa sasa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Fatma Hassan Toufiq aliyetaka kujua mkakati wa serikali kuhakikisha mafuta ya kula yanazalishwa kwa wingi.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kutekeleza mkakati wa kuendeleza sekta ndogo ya alizeti na chikichi ambayo ndiyo mazao makubwa yanayoweza kuzalisha kwa tija mafuta ya kula hapa nchini kwa sasa.

“Katika utekelezaji wa mkakati huo, viwanda vipya, kama Qstec na Jeolong vimeanzishwa; upanuzi wa viwanda kama Mount Meru Millers; pia serikali imeongeza nguvu katika taasisi za utafiti wa mbegu na hivyo kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za alizeti na michikichi.

“Mheshimiwa Spika, kwa sasa serikali imeelekeza nguvu zaidi kwenye kilimo cha kuzalisha mbegu bora, ili kukidhi mahitaji ya malighafi katika viwanda vyetu vya ndani,” amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments