Nyakato yatangulia nusu fainali

 

KATA ya Nyakato imefanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano ya Angeline Jimbo cup baada ya kuifunga timu ya Sangabuye bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa  uwanja wa shule ya msingi Sabasaba wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Alphashery Masele katika dakika ya 10.

Kocha mkuu wa timu ya Nyakato Smith Swai ameipongeza timu yake kwa kupata ushindi. Amesema kwa sasa watajipanga ili waweze kushinda mchezo wao wa nusu fainali.

Amesema mwaka jana timu yao ilimaliza nafasi ya pili ila mwaka huu wamejipanga kuweza kutwaa ubingwa wa mashindano ya Angeline Jimbo cup 2023.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Ilemela Hassan Milanga amempongeza mbunge wa Ilemela Dk Angeline Mabula.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments