Rais Samia afanya uteuzi wakuu wa wilaya, wakurugenzi

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Mwanahamisi Athumani Munkunda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara akichukua nafasi ya Hanafi Msabaha ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Mwanahamisi aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke na uteuzi wake ukatenguliwa na nafasi yake ikachukuliwa na Mobhare Matinyi.

Rais Samia amemteua Dk Stephen Isaac Mwakajumilo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu akichukua nafasi ya Mariam Chaurembo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Hassan Bakari Nyange ameteuliwa kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara TC, kabla ya uteuzi huu, Nyange alikuwa DAS Wilaya ya Namtumbo na anachukua nafasi ya Kanali Emmanuel Mwaigobeko ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Rais Samia pia Ametengua uteuzi wa Tatu Said Issike, Mkurugenzi wa Mtwara DC na kumteua Abeid Abeid Kafunda kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara DC, kabla ya uteuzi huu, Kafunda alikuwa mwanasheria katika ofisi ya mkemia mkuu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments