REHEMA ATAJA HOJA TANO USHINDI WA KISHINDO KWA CCM MBARALI

 IKIWA imesalia siku moja wananchi wa Jimbo la Mbarali mkoani kumchagua mbunge wao katika uchaguzi mdogo wa ubunge, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Rehema Sombi ametaja hoja tano zitakazoibeba CCM kushinda kwa kishindo


Rehema ameeleza hayo leo Septemba 18, 2023 katika Jimbo la  Mbarali wakati wa kampeni za mwisho kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika kesho.

Akizitaja hoja hizo Rehema alisema ya kwanza ni Serikali za CCM zimeendelea kutekeleza ahadi ilizozitoa katika uchanguzi mkuu wa mwaka 2020 kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa ufanisi wa hali ya juu.

Hoja nyingine alisema hadi sasa hakuna chama cha siasa kingine mbali na CCM ambacho kina hoja za msingi ambazo zimeshidwa kutekelezwa na serikali katika Wialaya ya Mbarali na  Jiji la Mbeya kwa ujumla.

"Wananchi ni mashahidi hoja za wapinzani kwa sasa ni kudai katiba mpya lakini sisi CCM tunaisukuma serikali ilete maji, ilete ajira kwa vijana kupitia kilimo. Mnaona msimamo wa serikali kupitia BBT, tunavyosukuma ajenda za barabara," amesema

Ametaja hoja ya tatu kuwa CCM imeendelea kuijenga Tanzania misingi ya umoja, mshikamano na amani ya taifa, hivyo kinaendelea kuwa chama tegemezi kwa taifa.

Hoja nyingine ni CCM ndicho chama pekee hadi sasa kilichobeba ajenda za kweli za ustawi wa jamii kwa wananchi katika kila sekta.

Pia, amesema hoja nyingine ni CCM kuwa  kiwanda cha viongozi bora, waliofunzwa, wazalendo, wanaojua umoja na misingi ya amani.
  


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments