Robertinho: Dynamos wajue Simba ni kubwa

KABLA ya mchezo wa kesho Ligi ya Mabingwa Afrika, kati ya Simba SC na Power Dynamos, Wazambia wanatakiwa kujua timu hiyo kutoka Msimbazi ni kubwa Afrika kwa sasa.

Hayo ni maneno ya kocha wa Simba, Robertinho alipozungumza mchana wa leo kuelekea mchezo huo utakaopigwa nchini Zambia saa 10 Alasiri kesho.

Robertinho amesema: “ Tunakwenda kucheza vizuri na kupata matokeo kwenye mchezo huu, kama tulivyofanya msimu uliopita.” amesema Robertinho.

Sambamba na hilo, kocha huyo amekiri kuwa michezo ya Ligi ya Mabingwa inakuwa migumu hata hivyo lengo lake ni kupambana kupata matokeo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments