ROTARY YAMWAGA TENA MADAWATI SHULE ZA MSINGI DAR

 KLABU ya Rotary ya Dar es Salaam imekabidhi madawati 100 kwa shule ya msingi Mtakuja manispaa ya Kinondoni na kufikisha idadi ya madawati takriban 2,500 yenye thamani ya takriban shilingi milioni 400 ambayo yameshatolewa na klabu hiyo kwa shule mbalimbali za msingi mkoani Dar es Salaam.


Madawati hayo yalikabidiwa hivi karibuni na wanachama wa klabu ya Rotary ya Dar es Salaam wakiongozwa na Gavana wa Kanda wa Rotary, Ssemwanga Francisco na kupokelewa na waalimu, wazazi na wanafunzi wa shule ya Mtakuja kata ya Kunduchi wakiongozwa na mwalimu mkuu wa shule ya Anna Nyomeye.  

Akikabidhi madawati hayo, gavana Ssemwanga amesema klabu ya Rotary ya Dar es Salaam kwa muda mrefu sasa imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuboresha huduma za jamii na mradi wao mkubwa wa jamii ni kusaidia katika sekta ya elimu kwa kuchangia madawati.  

Kwa upande wake, Mkuu wa shule hiyo Anna Nyomeye ameishukuru klabu hiyo na kwa mchango huo mkubwa na kuahidi kuwa uongozi wa shule utahakikisha kuwa madawati hayo yanatunzwa ili yadumu muda mrefu na kusaidia wanafunzi wengi kwa mika mingi.  

Kwa kutoa madawati hayo takriban 2500, Rotary imewapatia madawati wanafunzi zaidi ya 7,000 hivyo kuwaondolea adha ya kusoma wakiwa wameketi kwenye sakafu.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments