Samia aagiza ujenzi viwanja viwili vya kisasa

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kufanya maandalizi ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya ju viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma.”

Maagizo hayo yamekuja baada ya leo Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupitisha ombi la nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2027.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa ya soka Afrika (AFCON2027), tukishirikiana na Kenya na Uganda.” Ameandika Rais Samia kupitia mtandao wa X.

Rais Samia amewapongeza wote walioshiriki kuhakikisha Tanzania inapata fursa ya kushiriki michuano hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments