Samia atoa miezi sita changamoto ya umeme

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amempa miezi sita Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO) Gissima Nyamo Hanga kusimamia ukarabati wa mitambo ya umeme inayosababisha changamoto ya mgao.

Akizungumza leo Ikulu Dar es Salaam katika hafla ya uapisho wa viongozi wateule, Rais Samia amesema baada ya muda huo asisikie tena shida ya umeme.

“Nenda kaanzie pale Maharage alipofikia, najua utaweza, nakupa miezi sita nakuangalia pale Tanesco, kazi yako ya kwanza ni kusimamia ukarabati wa hiyo mitambo.” Amesema Rais Samia.

Rais Samia ametaja sababu inayopelekea uwepo wa changamoto ya umeme kuwa ni mitambo kwa muda mrefu haijafanyiwa huduma na kwamba itafanyiwa huduma kwa pamoja na ni lazima mitambo mingine iwake mingine izime, “kwahiyo tuna upungufu wa umeme.” Amesema Rais Samia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments