Samia: Kuokoa maisha ya watu hakutaki starehe

Rais Samia Suluhu Hassan leo amezindua Hospitali ya Kanda ya Kusini iliyopo mkoani Mtwara, huku akiwasisitiza watoa huduma za afya, kuzingatia maadili ya taaluma hiyo kwa kuwa wana jukumu kubwa la kuokoa maisha watu.

Katika kuweka msisitizo kwenye suala hilo amewataka watoa huduma hao, kutambua kuwa Mungu amewateua kwa ajili ya kuwasaidia watu hivyo wakati wote wanapaswa kuwa tayari kutimiza hilo.

“Niwaombe pamoja na changamoto zilizopo Mtwara, kazi inayofanyika hapa ni kuokoa maisha ya watu, kwenye kuokoa maisha ya watu, hatutaki starehe; siyo lazima kuwe na mji wenye mabaa, disco au mambo mengine, muhimu ni vifaa.


“Serikali imejitahidi vifaa vipo na ninampa jukumu Waziri wa Afya, akatafute fedha awaletee vifaa vya teknolojia kama vishkwambi. Tunachohitaji kutoka kwenu, mtunze jengo na vifaa vilivyopo ili huduma kwa wananchi itoke vyema,” amesema.Rais Samia yupo mkoani Mtwara ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku nne mkoani humo ambapo anatarajiwa kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments