Recent-Post

Samia: Ongezeni kasi zao la mwani

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka wakulima wa zao la mwani na wanaofanya shughuli za uvuvi katika Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi kuzalisha kwa tija ili kujiongezea kipato.

Rais Samia amesema hayo leo Septemba 19, 2023 alipokabidhi boti 34 kwa wavuvi na wakulima wa mwani zilizotolewa kwa   mkopo wa masharti nafuu.

Amefafanua kuwa boti hizo zipo 160 zimegharimu Sh bilioni 11.5. Amewataka wavuvi hao kutunza vifaa hivyo .

Amesema boti hizo zitawarahisishia kazi zao wakati wa kupanda, kuvuna na kubebea mizigo hadi nchi kavu.

Aidha amewataka wavuvi wazalishe samaria kwa wingi kwa kuwa kuna soko la uhakika.

Post a Comment

0 Comments